top of page

Kuhusu

Shield Our Watoto (SOW) ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo kuwa na faida ambalo linafanya kazi yake kushirikiana na wazazi/walezi husika, waelimishaji; taasisi za kidini, wizara husika, mashirika yanayohusiana na huduma za kijamii, NGOs, wanaharakati wa haki za binadamu na mashirika mengine ya utetezi wa watoto ili kukuza mazingira safi na salama kwa ubora wa watoto wetu kwa kushughulikia ukiukaji wa kijinsia na kuhimiza  uhusiano bora katika jamii.

SOW inaamini kwamba midahalo mbalimbali inayohusiana na ukatili au unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto inaweza kusaidia kuondoa tamaduni kandamizi kupitia kuelimisha watu ili kulinda watoto ndani ya jamii dhidi ya ukatili. 

Tunaamini kwamba sasa ni wakati wa kufanya jambo sahihi; tukomeshe ukatili na tulinde watoto wetu dhidi ya ukiukwaji huu usioelezeka. 

Dhamira Yetu

Kuanzisha mazungumzo ya kimataifa kati ya washika dau kuhusu unyanyasaji wa watoto kupitia elimu na uwezeshaji.

Kuanzisha taratibu endelevu ili kutekeleza kanuni bora zilizowekwa ambazo zita wawezesha watoto kuishi na kukua katika mazingira salama. 

iStock-484868534.jpg
Our Mission
Children in Science Class

Maono Yetu

Mazingira salama katika jamii yetu ambapo watoto wetu wanaweza kukua wakiwa na ujasiri na usalama.

Tunahitaji Usaidizi Wako Leo!

bottom of page